Tuesday, 5 July 2016

JAMAL KISONGO AELEZE YA MBWANA SAMATTA KWENDA AS ROMA

Good news kwa watanzania wote kwa mwaka 2016 ilikuwa ni headlines za nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa StarsMbwana Samatta kujiunga na KRC Genk ya Ubelgiji, lakini leo July 5 2016 jina la Samatta limerudi tena kwenye headlines za usajili.
Kuanzia usiku wa July 4 hadi leo July 5 habari zilizokuwa zimesambaa katika mitandao ya kijamii kuhusu Samatta ni kuwa yupo njiani kujiunga na klabu ya AS Roma ya Italia, hii ni taarifa ambayo imeenea kwa kiasi kikubwa hata kufikia baadhi ya wanasokaTanzania kutumia social network zao  kumpongeza.
sama 1
Mchezaji wa Yanga Haruna Niyonzima
Baada ya habari hii kuenea kwa kiasi kikubwa, alipotafutwa meneja wa staa huyo Jamal Kisongo atueleze ukweli wa taarifa hizo alisema “Huo ni uzushi tu hata sijui umetoka wapi na mimi nimesikia mitandaoni, lakini nimewasiliana na Samatta hakuna habari kama hizo wala mawakala wake hawana taarifa hizo”
sama 2

Labels:

0 Comments:

Post a Comment

Nawapenda

Subscribe to Post Comments [Atom]

<< Home