Marriage is a commitment, it's not a show of playing off
Jikite katika mambo ambayo yatafanya Ndoa idumu. Mambo ya pre wedding shoots, sare za maids, magari ya kifahari, ukumbi wa mamilioni, chakula cha gharama, zawadi za kujaza nyumba, na mengineyo hayana maana kama hutotilia mkazo katika mambo yatakayofanya ndoa idumu.
Kwani baada ya harusi mtakaobaki ni wewe na mpenzi wako, watu wote wataendelea na mishe zao. Mjue vizuri mpenzi wako kabla hamjaingia kwenye Ndoa, muwe marafiki, na ukumbuke kumtanguliza Mungu.
Pia usioe au kuolewa na mtu kwa sababu kwao wako vizuri kiuchumi. Kwamba utafurahi kuwa shemeji zako ni watoto wa waziri fulani, au mama mkwe wangu ni mkuu wa mkoa, au Baba mkwe ni mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CIG).
Hivyo vyeo havitafanya ndoa yako idumu, hata hvyo hao wamefanya bidii kufikia hapo walipo kwaiyo hata wewe unatakiwa kupambana na kusaidiana na mwenzako kufikia hatua njema.
Marriage is a commitment, it's not a show off, don't focus on the destination....work on the journey.
Badhi ya picha mbalimbali zikiwaonyesha wapambe na wanandoa wakifurahia siku yao ya harusi.
Labels: Udaku
0 Comments:
Post a Comment
Nawapenda
Subscribe to Post Comments [Atom]
<< Home