Tuesday, 5 July 2016

WEMA, DIAMOND WAKACHA BIFU SASA KUNOGESHA MTANDAO WAO


 Ni July 5, 2016 ambapo Staa Diamond Platnumz aliingia kwenye headlines mitandaoni baada ya kupost show ya Ex wake Wema Sepetu huku mashabiki wakawa na maswali mengi juu ya post hiyo.
Alipokuwa akihojiwa na Ayo Tv Wema Sepetu aeleze tofauti zake na Ex wake Diamond………..’Watu wamekuwa wakiitumia hii beef yetu kujipatia followers hasa kwenye mitandao yao kwasababu mtu anaweza akatokea sehemu yoyote na kuanza kunitukana mimi au kumtukana Naseeb akajipatia followers wa kutosha, kuna muda mimi nilikuwa naogopa kuimba wimbo wa Diamond unapopigwa naogopa hata kucheza’– Wema
Nikisikia nyimbo za Naseeb siwezi kuimba inanibidi nikaze lakini mwisho wa siku najikomoa mimi mwenyewe nikikaa kwenye gari nitaimba kama utakuwa unakumbuka nilivyoimba mara ya kwanza watu wakashangaa wakawa wanajiuliza maswali mengi sana, kwasasa hatuko kwenye mapenzi lakini tunasaidiana vitu kazi kuonesha uzalendo’– WemaWema.

Hii hapa chini ndio picha aliyoipost diamond huko instagram


Labels:

0 Comments:

Post a Comment

Nawapenda

Subscribe to Post Comments [Atom]

<< Home