Tuesday, 5 July 2016

SO SAD SHE LOST HER HUSBAND IN ONE SECOND BEFORE MARRIAGE

BASED ON TRUE LIFE STORY

Fikiria ile furaha unayoipata pale unapokuwa unafunga ndoa. Ni faraja ya pekee sana moyoni. Hua ni wakati muhimu sana hasa kwa wanawake kama wanaolewa na mwanaume aliyempenda na aliye chaguo lake.

Ila hii ilikuwa tofauti kwa mwanamke mmoja, alikuwa akikaribia kufunga ndoa na mwanaume alie dumu nae ktk urafiki kwa miaka sita, baada ya maandalizi ya muda mrefu sasa walikuwa wakisubiri ile siku muhimu.

Ilikuwa ni siku moja kabla ya harusi yake, ndipo alipopokea simu na kupata taarifa kwamba mume wake mtarajiwa, kipenzi chake amefariki kwa ajali ya gari wakiwemo na shemeji zake waliojeruhiwa

Mwanamke alizimia baada ya kupata taarifa zile, hata alipozinduka alichokua akikizungumza ni kuulizia aliko mume wake kwani hakuamini kama kweli amefariki. Yuko wapi mume wangu, yuko wapi Jay wangu, yuko wapi Jay wangu!! Haiwezekani aniache hivi...nitamfuata aliko!

Na hivyo ndivyo sherehe yake ya ndoa ilivyogeuka na kuwa msiba mzito!

____________________________________________

Nachukua nafasi hii kukuombea wewe rafiki yangu unaenisoma kila siku katika blog hii, kwamba hila za mwovu shetani zisikaribie upande wako. Muda wa furaha usigeuke kuwa huzuni kwako. Lengo la Mungu likatimizwe kwako. Hutakufa bali utaishi, uishuhudie ile kweli ya Mungu wetu aliye mkuu.

Kama una amini Tushirikiane pamoja kusema 'AMEN'

Labels:

0 Comments:

Post a Comment

Nawapenda

Subscribe to Post Comments [Atom]

<< Home