Saturday, 2 July 2016

MAKONDA AHAPA KULALA NAO MBELE MASHOGA DAR

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda  

Kwa ufupi:

Makonda amesema vitendo hivyo vimeanza kuongezeka jijini humo na lengo lake ni kuwaokoa watoto wasiige mambo hayo yanayoonekana kukua kwa kasi.

Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametangaza operesheni ya kuwasaka mashoga jijini humo.

Makonda amesema vitendo hivyo vimeanza kuongezeka jijini humo na lengo lake ni kuwaokoa watoto wasiige mambo hayo yanayoonekana kukua kwa kasi.

Bosi huyo wa mkoa amesema, “hili ni tatizo linalokua kwa kasi sitaruhusu liendelee katika mkoa wangu, nitawasaka popote walipo”.

“Hata hapa bandari wanaweza kuwapo mashoga wafichueni, mkiona mtu ana tabia za ajabu ajabu mfichueni, tutashughulika nao”, alisema.

TOA MAONI YAKO

Labels:

0 Comments:

Post a Comment

Nawapenda

Subscribe to Post Comments [Atom]

<< Home